Video: BAVICHA wazungumzia uchaguzi Arusha

Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), kupitia Mwenyekiti wao mpya, Patrick Ole Sosopi amekiri kuwa ni kweli mawakala wao walitolewa na polisi nje ya vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi mdoggo wa madiwani uliofanyika Novemba 26 mwaka huu.

“Wakati huu wa sasa akiwa kama Mwneyekiti tumeona na tumeonewa kama nilivyoeleza hatuko tayari kuonewa tena na wasihi vijana na kuwataka wajitetee inapobidi kujitetea hata sheria za nchi yetu zinaruhusu. Arusha ni kweli tumeona hiyo kadhia ya mawakala wetu kutolewa na polisi nje ya vituo ina prove ni jinsi gani maelekezo hayo yametokewa na maagizo kutoka juu polisi hawahusiki katika jambo lolote la uchaguzi wanapaswa kulinda vituo tena kwa kukaa nje,” amesema Sosopi.