Polepole awaponda Chadema, adai wamefulia.

Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema  CHADEMA wamefanya kikao cha dharura  kususia uchaguzi wa marudio wa majimbo na kata unaotarajiwa kufanyika January 13 mwakani.

Polepole amewatuhumu  CHADEMA  kuwa wanatumia mgongo wa kuminywa kwa Demokrasia nchini kususia uchaguzi huo wakati ukweli ni kwamba wamefulia baada ya kutumia vibaya hela ya mfuko wa chama chao.
“Watani wanakutana leo, agenda ni kutoshiriki uchaguzi unaokuja wa marudio kwa kisingizio cha demokrasia lakini ukweli ni matumizi mabaya ya fedha yamefuja mfuko wa chama. Tafuteni visingizio vingine lakini sio demokrasia. Watu wamechoka siasa za matukio. Kikao chema!” Ameandika polepole katika ukurasa wake wa Twitter.
==>Angalia hapo chini alichoandika