Manchester City waendeleza ubabe dhidi ya United.

Klabu ya Manchester City imeendeleza ubabe wake kwenye ligi kuu soka ya England baada ya kumchapa hasimu wake wa jiji moja Manchester United goli 2-1.

Kwenye mchezo huo ambao City ilimiliki mpira wakati mwingi, ilipata goli lake la kwanza kupitia David Silva dakika ya 43 kabla ya Marcus Rashford kusawazisha dakika ya 45 na baadae Nicolás Otamendi kupachika la pili na la ushindi kunako dakika ya 54.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwa sasa ni wazi asilimia kuwa ya ubingwa wa EPL msimu huu ukaenda kwa City.

Wamecheza vizuri, wengi walitarajia hili, ni vigumu kuwakabili kama hauna timu imara zaidi yao, tumemkosa Pogba ambaye angeweza kuleta madhara kwao, nafikiri wanaweza kuwa mabingwa msimu huu.’‘ amesema Mourinho kwenye mahojiano yake baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana.

Kwa misimu miwili mfululizo Manchester City imefanikiwa kushinda michezo miwili ndani ya dimba la Old Trafford na hakuna timu iliyofanya hivyo.