Ad imageAd image

KDN wafanya mkutano mkuu wa Mwaka 2024.

Togoro Media
1 Min Read

Leo Desemba 7 Umoja wa watoto wa Karukekere Kata ya Namhula wilaya ya Bunda DC wanaoishi nje ya Kijiji hicho wakiwa wamekutana ikiwa ni mara ya nne tangu umoja huo kuundwa.

Karukekere Development Network (KDN) iliundwa mnamo mwaka 2021 ikiwa na lengo la kusaidiana katika matatizo mbalimbali lakini pia kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo katika kijiji hicho.

Mpaka sasa KDN imekwisha fanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kijiji cha Karukekere ikiwemo ujenzi wa chumba cha akina Mama cha kujifungulia (Labour Room), Ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Sekondari pamoja kuchimba kisima kirefu cha maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa Karukekere chenye thamani ya Shilingi 24,417,000 ikiwa ni mradi walioutekeleza kwa kushirikiana na wahisani AZIMUT ONLUS.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Ndg, Daniel Ngawa amesisitiza suala la ahadi iliyotolewa na KDN kununua mashine ya kuburuzia (Photocopy Machine) katika Shule ya Sekondari Karukekere ikamilike mapema ili wanafunzi wa shule hiyo waweze kupata mazoezi mengi baada ya mada kuisha ili kujiandaa vizuri na mitihani yao hasa ngazi ya Taifa.

- Advertisement -
Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *