Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema atagombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho ambao amekuwa akihudumu kwa takriban miaka 20.
Mbowe aliwaomba wanachama na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kumpa saa 48 ili kuamua ikiwa atagombea nafasi hiyo baada ya wanachama hao kukusanyika kwenye makazi yake kumshawishi agombee.


