Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, leo Aprili 9, 2026 amewaapisha Wabunge wateule Mhe. Angela Kizigha pamoja na Mhe. Dkt. Eveline Wilbard Munisi Bungeni jijini Dodoma. Hapo wali Mhe. Angela Kizigha, alikuwa mmoja wa wasaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Eveline Wilbard Munisi, alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi na mgombea mwenza wa Urais kupitia tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.


