Ad image

Kambarage Wasira Aupata Ubunge, Amshukuru Rais Samia

Togoro Media
1 Min Read

Mhandisi Kambarage Masato Wasira amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Amesema anamshukuru kwa Imani kubwa aliyoionesha kwake kupitia mchakato wa ndani wa chama. “Ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa imani na heshima aliyonionesha”.

“Aidha, ninatoa shukrani za pekee kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kunichagua na kuniamini kuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la Afrika Mashariki”.

Wasira ambaye aliwahi kutia nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini na Kamati Kuu kutopitisha jina lake, amesema ataibeba nafasi hiyo kwa uadilifu mkubwa.

- Advertisement -

“Imani yenu ni dhamana kubwa kwangu, nami nitaibeba kwa uadilifu, weledi na uzalendo wa hali ya juu.Vilevile, napenda kukishukuru Chama changu, Chama Cha Mapinduzi, kwa kunilea kisiasa na kunijengea misingi imara ya uongozi na uwajibikaji”.

“Ninawaahidi Watanzania wote kuwa nitatumia nafasi hii kulinda na kutetea maslahi ya Taifa letu, kukuza ushirikiano wa kikanda, na kuchangia maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa manufaa ya wananchi wetu”. Amesema Kambarage

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *