Ad image

CCM Yawahimiza Vijana kugombea nafasi za Uongozi.

Togoro Media
1 Min Read

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi huku kikiahidi kuwapa fursa kwa kuwapitisha kwa kuwa wanao uwezo wa kuongoza.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana katika mkutano mkuu maalumu wa ukaribisho wa wananchama wapya 1,167 wa Seneti ya Vyuo Vikuu wa DIT, CBE, IFM na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kutoka tawi la Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki.

Kinana alisema Chama kinawategemea vijana kwa kuwa wanayo chachu ya mawazo kwa Chama, hivyo wasifikiri kuwa kuna sehemu nyingine mawazo yatatoka bali watambue kuwa wao ni taifa la leo.

Alisema Chama kinawategemea kwa ushauri, kujenga hoja na kukosoa, hivyo watambue wao ni watu wa kisasa, wasomi na wanakwenda na kasi ya upatikanaji wa taarifa hususan kupitia mitandao ya kijamii.

- Advertisement -

“Kutokana na hilo mnao uwezo mkubwa wa kutushauri, kutujenga na kutukosoa, tunakutegemeeni sana, toeni mawazo. mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mitaa, nawasihi vijana jitokezeni na gombeeni katika nafasi zote,” alisema Kinana.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *