Afisa Kilimo katika kata ya Neruma wilaya ya Bunda mkoa wa Mara anayefahamika kwa jina la Julius Rubambi (38) ameuawa kwa kuchomwa kisu na kung’atwa ulimi na mkewe kutokana na wivu wa kimapenzi huku mkewe Elizabeth Stephen (36) akijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya Kibara.
Inasadikika kuwa chanzo cha ugomvi huo ni mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa ameanzisha mahusiano mengine nje ya ndoa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mara ACP Salim Morcas amesema tayari mwanamke huyo anashikiliwa na Jeshi hilo na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.


