Shambulio moja limetokea eneo la Palm Jumeirah nchini Dubai.
Kwa mujibu wa ofisi ya habari nchini humo, vikosi vya uokoaji vilitumwa mara moja katika eneo la tukio na moto uliotokana na tukio hilo na kufanikiwa kuudhibiti na kusababisha Watu wanne kujeruhiwa na wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.

Taarifa hiyo inafuatia ripoti ya awali ya shahidi wa tukio, iliyosambazwa pamoja na picha inayoonyesha moshi katika eneo hilo, baada ya vyombo vya habari vya serikali ya Iran kudai kuwa shambulio lilikuwa limeanzishwa dhidi ya Dubai.
Haijabainika wazi Iran inalenga nini hasa, ingawa kuna uwepo wa kijeshi wa United States katika nchi hiyo.

Palm Jumeirah ni visiwa bandia vinavyojulikana kwa hoteli za kifahari na makazi ya hali ya juu.
Chanzo: East Africa TV

