Ad image

Wawili Wahukumiwa Maisha Kwa Kubaka

Togoro Media
1 Min Read

Mahakama ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma imewahukumu Idd Abubakari Waitara (20) na Mabuda Ally Issa (20), wote wakazi wa Kijiji cha Jangalo, kwenda jela maisha na kuchapwa viboko kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kubaka kwa kundi.

Tukio hilo lilitokea kati ya Agosti 5 na 8, mwaka 2025 ambapo watuhumiwa hao walimbaka mwanamke mmoja. Washitakiwa walikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo walisomewa mashitaka na kupatikana na hatia.

Hukumu hiyo ilitolewa Februari 27, 2026 mbele ya Hakimu Mheshimiwa Hayuma.

- Advertisement -
Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *