Ad imageAd image

KATAVI: Mwalimu Aidan Ramadhani Achinjwa Kama Mnyama

Togoro Media
1 Min Read

Mwalimu wa Shule ya Msingi Nguvumali mkoani Katavi, anaejulikana kwa jina la Aidan Ramadhani anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 hadi 43 ameuwa kikatili kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili, na mwili wake kutupwa katikati ya Mtaa wa Mkwajuni Kata ya Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Tukio hilo la kusikitishwa limetokea usiku wa kuamkia Machi 20, ambapo wananchi walipigwa na butwaa kuuona mwili wa mwalimu huyo ukiwa umetenganishwa kichwa na Kiwiliwili

Amos Mkingwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkwajuni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kubaini waliotekeleza mauaji hayo ya kinyama.

Amesema kuwa tukio hilo limewasikitisha wananchi wa Mtaa wa Mkwajuni kwa kuwa ni tukio lisilo la kawaida.

- Advertisement -

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *