Polisi Mkoa wa Mara inamshikilia Mwanasheria Keneth Nkiko (28) ambaye jukumu lake lilikuwa kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambaye anatuhumiwa kumuua Magreth Richard (22), mfanyabiashara na mkazi wa Manispaa ya Musoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amesema tukio hilo limetokea saa 4 asubuhi ya jana Jumatatu, Oktoba 5,2026 katika Mtaa wa Mwigobero, Manispaa ya Musoma
Kamanda Lutumo amesema Nkiko anadaiwa kumuua dada huyo ambaye alikuwa ni mpenzi wake kwa kumpiga na kitu butu kichwani kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha
Alimpiga na kitu butu kichwani kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali na kusababisha majeraha mengi mwilini yaliyosababisha avuje damu nyingi na kufariki papo hapo,” amesema
Amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mpenzi wake huyo kuwa na mahusiano na wanaume wengine.

