Walimu wa shule ya msingi Nyansalala iliyopo kata ya Bukondo Halmashauri ya wilaya ya Geita, wamelazimika kufanya kazi wakiwa wamekaa chini baada ya kamati ya shule na uongozi wa kijiji hicho kuwanyang’anya madawati waliyokuwa wakiyatumia ofisini kama mbadala wa viti na meza.
Akielezea tukio hilo mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwalimu Joseph Mfungi amesema alipigiwa simu na Mwalimu Mkuu Msaidizi kuwa Afisa Mtendaji wa kijiji hicho amewataka walimu kuwapatia wanafunzi madawati waliyokuwa wanakalia kwani madawati hayo yameletwa kwa ajili ya wanafunzi.
Chanzo: EATV


