Ad imageAd image

Wachimbaji wadogo Kinyambwiga wailalamikia Serikali ya Kijiji.

Togoro Media
1 Min Read

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wapatao 3,000 katika Mgodi wa Kinyambwiga uliopo Wilayani Bunda mkoani Mara, wameandamana na kuzingira Ofisi ya serikali ya Kijiji cha Kinyambwiga wakiwa na mabango wakiitaka serikali kuwarudishia maeneo waliyokuwa wakichimba.

Hatua hii imekuja baada ya serikali kuwaondoa kwenye maeneo yao kutokana na kufanya shughuli za uchimbaji kwenye Leseni ya mtu mwingine bila kufuata utaratibu huku wakidaiwa kutorosha madini hayo.

Vurugu zimeibuka katika eneo hilo la Kinyambwiga baada ya serikali kuwaondoa wachimbaji wadogo katika eneo hilo kumpisha mwekezaji pamoja na mmliki wa leseni anayetambukika kwa jina la John Bina kuendelea na uchimbaji.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *