Madaktari sita wa Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza wamejeruhiwa baada ya gari walilopanda kupata ajali katika Kijiji cha Maremwe, Kata ya Igongwa, wilayani Kwimba wakati wakitoka kutoa huduma kwenye kambi ya matibabu ya kibingwa katika Hospitali ya Icheja.
Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema kwamba ajali hiyo imetokana na dereva kujaribu kumkwepa mwendesha baiskeli aliyekuwa ameanguka barabarani.


