Ad image

Mamia Wajitokeza Kumzika Njiwa Manga

Togoro Media
1 Min Read

Msanii wa nyimbo za asili kutoka Butiama Mara, Njiwa Manga, leo amezikwa katika makaburi ya familia huko Butiama Mkoani Mara katika kijiji cha Buturu.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na mamia ya mashabiki zake kutoka maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa ikiwa ni mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza na Shinyanga.

Njiwa Manga alifariki tarehe 07/06/2026 Wilayani Butiama ambako alilazwa hospitalini kwa siku kadhaa hadi umauti ulipomkuta. Alijipatia umaarufu zaidi kwa wimbo wake uliojulikana kwa jina la “Sindika”.

Sisi TOGORO MEDIA tunaungana na ndugu jamaa na marafiki pamoja na mashabiki wote wa Njiwa Manga kuomboleza msiba huu mkubwa. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe AMEN.

- Advertisement -

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *