Ad imageAd image

Mzee Mwinyi apelekwa Hospitali Kwa kubanwa Kifua.

Togoro Media
1 Min Read

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua na anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia ya Mzee Mwinyi, Abdullah Ali Mwinyi  inaeleza kuwa kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu, hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala na Maombi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali” Amesema Abdullah Ali Mwinyi, Msemaji wa Familia.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *