Ad imageAd image

Mwalimu Herieth Lupembe auawa kikatili Mbeya.

Togoro Media
1 Min Read

Herieth Lupembe ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Mbugani na Mkazi wa Kiwanja kata ya Kiwanja Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya pamoja na mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela wameuawa na watu wasiojulikana huku mtoto mwingine mwenye umri wa miaka miwili akijeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali

Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni machi 31,2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia hakuonekana kanisani wakati si kawaida yake.

Akizungumza na vyombo vya habari,Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiwanja mahali alipokuwa akiishi mwalimu huyo, Gideon Peter Kinyamagiha amesema walifika nyumbani kwa marehemu na walipoingia ndani walikuta sururu ikiwa na damu na marehemu wawili na mtoto wa kiume wa mwalimu huyo akiwa amejuriwa

Mwenyekiti anasema baadaye walitoa taarifa Polisi ambao nao walifika na kufanya uchunguzi wa awali kisha kuchukua miili na kwenda kuihifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi ambapo majeruhi amekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.

- Advertisement -

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *