Leo Julai 5, 2024 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) na kuahidi kuwa Serikali itafanya nayo kazi kwa karibu ili iweze kufanikisha malengo ya Tanzania kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ina imani kubwa na kamati hiyo kwamba itapata mafanikio.


