Mwanamuziki nguli wa miaka mingi kwenye muziki wa dansi nchini, Kikumbi Mwanza Mpango maarufu kama King Kikii amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo.
Mzee King Kikii amefikwa na mauti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alilazwa kwa muda mrefu.
King Kikii atakumbukwa zaidi kwa wimbo wake maarufu unaojulikana kama “Kitambaa Cheupe”. Togoro Media inaungana na familia,ndugu,marafiki na Taifa kwa ujumla kuomboleza msiba huu mkubwa.
#RestEasyKing


