Mwana mitandao na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Niffer amekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kuchangisha fedha takribani Milioni 37 kwa watanzania kufuatia ajali ya Ghorofa iliyotokea Kariakoo mapema Jumamosi ya tarehe 16 Novemba.
Waziri mkuu, Mh. Kassim Majaliwa ametoa tamko la kukamatwa Niffer alipofika Kariakoo kushuhudia maendeleo ya shughuli za uokoaji na kuongeza kuwa mwanadada huyo aseme hizo fedha ametumwa na nani kuzichangisha na kibali amepewa na nani.


