Huyu hapa anaitwa Catherine Mtuya (Farpraud), Binti kutoka kabila la Chief Mkwawa, Mhehe na mzaliwa wa Iringa, mpenda michezo lakini zaidi anapenda mitindo, ndoto ambayo ameibeba na anaamini siku moja itatimia na atakuwa mwanamitindo mkubwa Duniani.

Farpraud kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru, mjasiriamali na mwanamitindo, Binti mwenye ndoto kubwa na anaamini kuna siku Dunia itamjua kupitia tasnia ya urembo na mitindo.

Mbali na mitindo, Farpraud pia anapenda muziki, anapenda kuimba na anasema anapenda zaidi muziki wa hip hop.



