Hello hello kizazi cha Bongo Fleva. Leo tumekuwekea mistari, pita nayo kisha uweke comment yako utuambie wakati huo ulikuwa wapi??
SIFAI – Q JAY FT JOSLIN (MJ RECORDS)
Mwanzo mi nilikuomba penzi
Ukasema we hutaki ushenzi
Nilikubembeleza tena sana
Baadaye ukakubali
Tulipendana tena kwa dhati
Wiki mwezi mwaka ulikatika
Nikagundua umebadilika
Ukaanza fanya mambo ya kishenzi
Nilikuonya hukutaka kusikia
Ukasema mi sifai
Ukasema hunitaki
Ukasema sina hadhi mimi mimiii
CHORUS
Anasema mi sifai
Anasema hanitaki
Anasema sina hadhi mimi mimiii ×2
Usiku kucha nakuwaza
Sili wala silali
Nakuwaza we mpenzi wangu
Kumbuka mi nakupenda
Ila we unanitenga
Bado mimi nakupenda
Nasisitiza nakupenda nasisitiza nakupendaa
Wazuri wapo wengi
Siwezi kukusaliti
Naomba uniamini naomba uniaminii
Tabia yako na umbo lako
Vilinifanya niwe na wewe baby lady
CHORUS
Anasema mi sifai
Anasema hanitaki
Anasema sina hadhi mimi mimiii ×2
Sijui kwanini anasema eti kwamba mi sifai yeah
Au sababu sina mali eti mimi masikini yeah
Hili naomba nijue ooh hilo naomba nijue ooh
Mi nasikitika inaniuma sana yeah
Wee haya wee haya wee haya wee haya
Anasema mi sifai anasema mi……
We hujui tuu jinsi gani moyo wangu unaumiza
Na hujui tuu jinsi gani nawaza
Yeah kwanza naumia moyoni
Ulivyokuwa unanipelekapeleka tu zamani
Haukuona kama unakosea
Tell me hukuona kama unapotea
Yeah mi naskia uchungu
Sure I love mom haki ya Mungu
Inafika kipindi nna gadhabu sana
Hasira nyingi mpaka nashindwa kusoma
Ooh hii yote kwa sababu yako
Kwakuwa ulikuwa tofauti na wenzako
Lakini poa tu fresh
We ulipenda shobokea wenye cash
Skiza saivi mimi nina mtoto mzuri
Ana macho mazuri ananfikisha mbali
Ana mapozi ya kweli ana tabia nzuri
Kwaiyo samahani sana tafadhali
CHORUS
Anasema mi sifai
Anasema hanitaki
Anasema sina hadhi mimi mimiii ×4
MJ
Q Jay
Wakali Kwanza


