Ad imageAd image

Mjue Pape Bouna Thiaw, Kocha Wa Timu Ya Taifa Ya Senegal.

Togoro Media
1 Min Read

Pape Bouna Thiaw, Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal
Jina Kamili: Pape Bouna Thiaw
Tarehe ya Kuzaliwa: 5 Februari 1981
Kazi: Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Senegal (Teranga Lions) tangu Desemba 2024

Thiaw alikuwa mchezaji wa kandanda aliyewahi kucheza nafasi ya mshambuliaji (forward). Alijipambanua katika vilabu mbalimbali barani Ulaya, akitumikia klabu za Ufaransa, Uswisi, na Uhispania, pamoja na mkopo na Dynamo Moscow nchini Urusi.

Alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Senegal, akishiriki na kufunga magoli kadhaa, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika FIFA World Cup 2002. Baada ya kuacha soka la kucheza, Thiaw alianza kazi yake ya ukocha na baadaye akawa kocha wa Senegal A’ (timu inayoundwa na wachezaji wa ligi ya ndani), na alishinda Kombe la African Nations Championship (CHAN) 2022.

Mnamo 13 Desemba 2024, aliteuliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Senegal baada ya kuondolewa kwa kocha aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Aliou Cissé. Thiaw ameiongoza Senegal kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026.

- Advertisement -

Mnamo 18 Januari 2026, ameweka kwa kuiongoza Senegal kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (Africa Cup of Nations) 2025/2026, ikishinda dhidi ya Morocco 1-0 kwa dakika za ziada.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *