Ad imageAd image

Wanaanga Wa Artemis II Warejea Duniani Salama

Togoro Media
1 Min Read

Wanaanga wa Artemis II wamerejea salama Duniani baada ya kutua kwa ustadi mkubwa wakihitimisha safari yao ya kihistoria ya siku tisa

Kikosi kilitua katika Bahari ya Pasifiki saa 01:07 BST (20:07 EDT), huku kamanda Reid Wiseman akithibitisha timu yake iko katika hali njema.

“Huu ni mwanzo wa enzi mpya ya uchunguzi wa anga wa binadamu,” NASA imesema baada ya kurejea kwa kikosi hicho

Wanaanga hao wanne “wanajisikia vizuri sana”, afisa wa matibabu amethibitisha, na walisafirishwa kwa helikopta kurudi kwenye meli ya jeshi la majini la Marekani kwa uchunguzi zaidi

- Advertisement -

Kikosi cha Artemis II kilifanikiwa kuingia tena kwenye angahewa ya Dunia baada ya kukatika kwa mawasiliano kwa dakika sita japo ni hali ya kawaida lakini ya kusisimua na yenye wasiwasi

Tarehe 6 Aprili, chombo hicho cha anga kilifikia umbali wake mkubwa zaidi kutoka Duniani — kilomita 406,771 (maili 252,756) — wakati wa kupita karibu na Mwezi, kikivunja rekodi ya awali ya umbali mkubwa zaidi ambao binadamu wamewahi kusafiri angani

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *