Mchezaji na kiungo fundi kutoka TP Mazembe na Timu ya Taifa ya Zambia, Chipolopolo, Rainford Kalaba amefariki dunia.

Taarifa zilizotufikia ni kwamba mchezaji huyo amepata ajali mbaya ya gari alilokuwa akiliendesha mwenyewe Lusaka Zambia baada ya gari lake kugongana uso kwa uso na lori na kufariki papo hapo.

