Ad imageAd image

Wafungwa zaidi ya 1000 wapata msamaha wa Rais.

Togoro Media
1 Min Read

Jumla ya wafungwa 1082, wamepata msamaha wa Rais leo ambapo 29 kati yao wameachiliwa huru leo Aprili 26, 2024.

Wafungwa 20 waliohukumiwa adhabu ya kifo wamebadilishiwa adhabu hiyo na kuwa kifungo cha maisha, wafungwa 27 waliohukumiwa kifungo cha maisha wamebadilishiwa kuwa kifungo cha miaka 30 na wafungwa 1006 wamepunguziwa adhabu zao na watabaki gerezani na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.

Msamaha huo umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka aliyopewa chini ya ibara ya 45(1)(a)-(d) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa msamaha kwa wafungwa, ikiwa leo ni maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

- Advertisement -

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *