Ad imageAd image

Baba Amuua Mwanae Kisa Pombe ya Posa.

Togoro Media
2 Min Read

Moshi, Kilimanjaro

Tukio la kusikitisha limetokea mkoani Kilimanjaro ambapo kijana mmoja amefariki dunia baada ya kushambuliwa na baba yake mzazi, kufuatia ugomvi uliotokana na pombe iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya sherehe ya posa ya familia.Marehemu ametambuliwa kwa jina la Mathias Laurian Teti (26), mkazi wa Kijiji cha Shimbwe Chini, Kata ya Uru Shimbwe, wilayani Moshi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, tukio hilo lilitokea asubuhi ya tarehe 21 Januari 2026, nyumbani kwa familia hiyo, baada ya kuzuka ugomvi kati ya marehemu na baba yake, Laurian Teti, kuhusu matumizi ya pombe iliyokuwa imenunuliwa kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya posa ya dada yao.

Inadaiwa kuwa ugomvi huo ulianza kwa maneno kabla ya kugeuka kuwa vurugu, hali iliyosababisha baba kumshambulia mwanae, na kumjeruhi vibaya hadi kusababisha kifo chake.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa tayari yupo mikononi mwa polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi.

- Advertisement -

“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hili, na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara taratibu za kisheria zitakapokamilika,” alisema Kamanda Maigwa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu (postmortem), huku jamii ikihimizwa kuepuka migogoro ya kifamilia na matumizi mabaya ya pombe yanayoweza kusababisha madhara makubwa, ikiwemo kupoteza maisha.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kutatua migogoro kwa njia za amani na kutoa taarifa mapema pale dalili za vurugu zinapojitokeza.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *