Bei ya mafuta duniani imepanda huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu iwapo makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran yatadumu baada ya Israel kuanzisha wimbi la mashambulizi dhidi ya Lebanon.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema vikosi vya nchi hiyo vitabaki katika eneo hilo hadi Iran itakapokubaliana na kuafikiwa kwa makubaliano “halisi” ya kusitisha mapigano.
Wasiwasi pia unaendelea kuongezeka kuhusu kama njia muhimu ya meli katika Mlango wa Bahari wa Hormuz utafunguliwa.
Siku ya Jumatano mara tu baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano, bei ya mafuta ghafi ilipanda kwa 2.7% siku ya Alhamisi kwa $97.23 kwa pipa.


