Ad image

Jela Miaka 30 Kwa Kumbaka Mpwa Wake.

Togoro Media
1 Min Read

Mwanaume mwenye umri wa miaka 40 amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Eldoret nchini Kenya baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumwambukiza mpwa wake wa miaka 10 virusi vya Ukimwi.

Mshukiwa alishtakiwa kwa kumnajisi mtoto huyo kwa tarehe zisizojulikana mnamo Septemba 2023 katika Kijiji cha Chemoru, Kaunti ya Uasin Gishu.

Wakati akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Eldoret Daniel Sitati alisema kuwa mashahidi watatu, ikiwa ni pamoja na ripoti ya matibabu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Moi (MTRH), ilithibitisha kuwa mshukiwa alitenda kosa hilo.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *