Ad image

Chivayo Na Mkewe Lucy Kuzikwa Kesho

Togoro Media
1 Min Read

Majeneza yenye miili ya Mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo na mkewe Lucy Muteke ‘Lulu’, yamefikishwa nyumbani kwao Jijini Harare kwa ajili ya ibada za mwisho kabla ya kuzikwa Oktoba 8, 2026

Wawili hao, waliofariki katika ajali ya helikopta Septemba 30, 2026, watazikwa wakiwa kwenye majeneza, tofauti na utaratibu wa kawaida wa dhehebu la Johane Masowe, ambalo Waumini wake huzikwa bila majeneza

Leo, Oktoba 7, 2026, Ndugu, Marafiki na Waumini wamekusanyika nyumbani kwa marehemu Chivayo Jijini Harare kwa ajili ya ibada na maandalizi ya mwisho kuelekea mazishini, huku Polisi wakifunga baadhi ya barabara zinazozunguka eneo hilo ili kurahisisha msafara wa magari

Chivayo na Lucy wanatarajiwa kuzikwa kesho, Oktoba 8, 2026, katika Makaburi ya Glen Forest Jijini Harare, Zimbabwe, kwenye makaburi mawili yatakayokuwa pembeni kwa pembeni.

- Advertisement -

Credit: Millard Ayo

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *