Mlipuko mkubwa wa gesi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, umesababisha vifo vya watu watatu na kuwajeruhi wengine 300.
Lori lililokuwa limebeba mitungi ya gesi lililipuka katika wilaya ya Embakasi majira ya saa 23:30 (20:30 GMT), na kuwasha moto mkubwa.


