Ad image

MABEYO: Hayati Joseph Magufuli alijua hatapona.

Togoro Media
2 Min Read

Ikiwa jana imetimia miaka 3 tangu Rais wa awamu ya Tano, Mh. John Pombe Magufuli kufariki, Mkuu wa majeshi mstaafu Venance Mabeyo ametoa siri aliyoificha kwa muda mrefu.

Mabeyo anasema “Kitu ambacho sijawahi kusema ni kuwa Rais John Magufuli aliniita akaniambia CDF njoo, akaniambia siwezi kupona. Waamuru hao madaktari wanirudishe nyumbani. Nikamwambia mheshima sina hayo mamlaka. Akasema CDF huwezi kuwaamuru wanirudishe nyumbani? Nikamwambia suala la afya si la CDF,” Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Venance Mabeyo anasimulia na kueleza kuwa alimshauri kuwa madaktari walikuwa wanaendelea vyema kumpambania.

Anasema, “Kujua hali yake ilivyo, tulienda kila asubuhi na jioni kumuona. Tulikuwa na nafasi yetu kama wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama tunashauriana…

“Badae tukampeleke Hospitali ya Mzena, pale kulikuwa na utulivu na tukaweka usalama pale na madaktari walipelekwa kumwangalia kwa wakati wote,” anaeleza

- Advertisement -

Mabeyo anasimulia kuwa siku moja kabla ya kifo cha Rais Magufuli, hali ilibadilika na yeye alitambua hali imebadilika.

Anasema, “Aliona hali yake na Mwenyenzi Mungu alimuonesha kuwa hatapona na alichosema nirudisheni nyumbani nikafie nyumbani tukamwambia hapa uko mikono salama.”

Baada ya kuona CDF ana msimamo wa kutoamrisha arudi nyumbani, akamwambia amuitie paroko wake wa Kikatoliki, paroko wa St Peters anaitwa Askofu Makubi na Kadinali Pengo.

“Hiyo asubuhi tulimtafuta Kadinali Pengo lakini alikuwa ibadani. Baada ya muda akaniuliza haujampata Pengo, nikamwambia alikuwa kwenye ibada ila nimeshamtumia usafiri na atafika.

“waliwasili na kumsalia kwa taratibu za kikatoliki. Walifanya ibada na kumpa sakramenti ya upako wa magonjwa kwa anayekuwa katika hatari ya kufariki. Alipumizka na ilipofika mchana saa nane, walitupigia na kutueleza hali ya Rais si nzuri. Tulimkuta na hakuweza kuongea,” anaeleza.

- Advertisement -

Mabeyo alisema Rais Magufuli aliendelea kupata tiba mpaka jioni. “Ilipofika saa 12 na nusu au saa moja kasoro akakata roho. Tulikuwa wakuu wa vyombo watatu, pale nilikuwa mimi, IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) na DGIS .

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *