Katika kusherehekea siku ya wafanyakazi, Mei Mosi mkoni Mara, Mkuu wa Mkoa huo Mhe, Kanali Alfred Mtambi amekemea vitendo vya ukatili na mauaji ya kiholela mkoani humo.

Katika hotuba yake pia amewaomba walimu, viongozi na wasanii wote mkoani humo kutumia nafasi zao katika jamii kutoa elimu kuhusu utokomezaji wa mauaji mkoni Mara.


