Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Mkurugenzi wa Emf pamoja na TVE majizzo ameandika ujumbe huu…
“Kwa moyo mzito na machozi mengi, nasikitika kutangaza kifo cha rafiki, kaka, aliyekuwa msimamizi wa ndoa yangu, na mfanyakazi mwenzangu aliyeitumikia EFM na TVE kwa nguvu zake zote, ndugu yangu Ssebo“.
Ssebo amefariki usiku huu katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Kwa sasa mturuhusu kuaanda taratibu zote zinazohusiana na msiba huu wa Ghafla, ambao kwa kweli siwezi kuuelezea.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. #RIPSsebo”


