Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (SERENGETI BOYS) imefuzu fainali ya AFCON U-17 na kuiondoa Misri kwenye mashindano hayo.
Katika mtanange huo Serengeti Boys ilimaliza kwa suluhu ya bila kufungana na Misri na hatimaye kupata ushindi kwa njia ya Penalti.
Timu hiyo sasa inasubiri mshindi kwenye mchezo kati ya Morocco na Senegal

