Mchekeshaji maarufu nchini, Pembe amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Temeke alipokuwa anapatiwa matibabu.
Akithibitisha taarifa hizo, rafiki wa karibu na Pembe, Senga ambaye wamefanya kazi pamoja kwa muda mrefu amesema marehemu Pembe alikuwa akikohoa na kubanwa kifua karibia wiki mbili zilizopita.


