Mwanahabari mkongwe na Mkurugenzi wa Haroub Media kutoka Mbeya ameweka wazi juu ya mijadala iliyoibuka kutoka kwa watu tofauti tofauti kuhusu umiliki wa nyumba yake mpya ya kifahari aliyoionesha hivi karibuni.

Katika ukurasa wake wa Facebook, mwanahabari huyo amechapisha picha za nyumba hiyo zikiambatana na hati ya umiliki huku akiandika ujumbe ambao unadhaniwa kuwa ni jibu kwa wale waliobeza na kudhania yeye siyo mmiliki halali wa nyumba hiyo.

Haroub Kabwe ni mwanzilishi na mmiliki wa Haroub TV lakini pia aliwahi kuwa Meneja wa kituo cha redio cha Mbeya FM.


